Home Burudani Ebwanae Shilole kahamia mjengoni kwake

Ebwanae Shilole kahamia mjengoni kwake

3534
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole, amesema amehamia rasmi katika mjengo wake mpya uliopo Majohe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Shilole, alisema anashukuru Mungu kuona baadhi ya mipango yake kwa mwaka huu ikitimia ikiwa ni pamoja na kuhamia kwenye nyumba hiyo ya kisasa.

Alipoulizwa ametumia kiasi gani cha fedha kukamilikakwa nyumba hiyo, Shilole, alipatwa na kigugumizi na kusema hapendi kuweka wazi hilo.

“Kikubwa ni kwamba nakaa kwenye nyumba yangu, hilo ndilo la kumshukuru Mungu, ukiniuliza nimetumia kiasi gani siwezi kukujibu kwa haraka kwa kuwa kama unavyojua pesa zetu za mawazo na nilikuwa nahanga ikanikipata kidogo naweka mpaka nilivyofika hapa,” alisema Shilole.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here