Home Michezo Kimataifa EDEN HAZARD: NI RAHISI KUSEMA SARRI NI BORA

EDEN HAZARD: NI RAHISI KUSEMA SARRI NI BORA

6244
0
SHARE

LONDON, England


NYOTA wa Chelsea, Eden Hazard, anasema Maurizio Sarri ni kocha mkubwa akisisitiza kuwa kila mmoja anaona anachokifanya kwa sasa klabuni hapo, ukiwa ni msimu wake wa kwanza.

The Blues wanaendelea kufurahia maisha mapya baada ya kushinda michezo mitano ya ligi kabla ya mwishoni mwa wiki kuambulia sare ya 0-0 dhidi ya West Ham, wakiongozwa na Sarri aliyechukua mikoba ya mtangulizi wake, Antonio Conte.

Hazard hakuwa kwenye kiwango cha kuridhisha sana msimu uliopita, ikitajwa hakukuwa na mahusiano mazuri kati yake na kocha wake, Conte na kuanza kuhusishwa kujiunga na Real Madrid.

Tangu kuwasili kwa Sarri, Hazard amerejea kwenye kiwango cha awali ambapo hadi sasa katika michezo sita iliyopita ya ligi, amekuwa mwiba mchungu kwa mabeki akitoa asisti mbili.

“Tunatengeneza nafasi za kutosha, tumekuwa na umiliki mkubwa wa mpira, tuna kocha bora nyuma yetu nakuhakikishia tuna kocha mkubwa duniani,” aliliambia Sky Sports.

Chelsea wanatarajia kushuka dimbani usiku wa leo kuvaana na Liverpool mchezo wa Kombe la Carabao, kabla ya miamba hiyo kunyooshana Jumamosi katika mwendelezo wa Premier League.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here