Home Michezo Kimataifa England wadaiwa kupanga matokeo

England wadaiwa kupanga matokeo

0
SHARE
Jan Durica

TRNAVA, Slovakia

BEKI wa Slovakia, Jan Durica, ameishtua dunia baada ya kusema wazi kuwa ushidi wa England dhidi yao ulikuwa umepangwa.

Mchezo huo ulipigwa katika jiji la Trnava na England kuibuka na ushindi wa bao 1-0, likiwekwa kimiani dakika za mwisho na staa wa klabu ya Liverpool, Adam Lallana.

Kwenye pambano hilo, Slovakia walilazimika kucheza kwa dakika 33 wakiwa 10 uwanjani, baada ya beki wao, Martin Skrtel kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Harry Kane.

Durica, aliyepangwa sambamba na Skrtel kwenye nafasi ya mabeki wawili wa kati, amesema ushindi wa England ulipangwa ili kuhakikisha wanafuzu Kombe la Dunia mwaka 2018, litakalofanyika Rusia.

“Kuna nafasi moja tu ya kufuzu kwenye kundi letu, unafikiri itakuwa ni rahisi kwa Slovakia kufuzu na kuiacha England?” aliuliza Durica.

“Bila shaka wangependa timu inayofahamika ifuzu na ninaamini kabisa waamuzi walifahamu mpango huu. Leo hatukucheza na England pekee, hivyo ndivyo ninavyoamini.”

Ushindi huo umewafanya England kushika nafasi ya pili kwenye kundi F, nyuma ya Scotland, walioichapa Malta bao 5-1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here