SHARE

LONDON, England


Wafahamu marefa watakaochezesha Ligi Kuu England na timu wanazoshabikia

JAMBO la ajabu, pengine la kipekee zaidi katika mchezo wa soka, ni utaratibu wa marefa wanaochezesha mechi za Ligi Kuu England kuwa huru kutaja timu wanazoshabikia.

Kwa bongo hii ni nongwa. Ukijulikana tu, hata kwa tetesi basi ni vyema ukasaka kazi nyingine ya kufanya. Urefa utakushinda.

Kuelekea msimu mpya wa Premier League 2018/19, DIMBA Jumatano tumekuandalia wasifu wa marefa wote watakaochezesha Ligi hiyo.

Martin Atkinson

Tarehe ya kuzaliwa: 31/3/1971

Mji: Bradford

Alijiunga Premier League: 2004

Timu anayoshabikia: Leeds

Mechi kubwa alizochezesha:

 • Fainali ya Kombe la FA 2011 – Manchester City 1-0 Stoke
 • Mchujo wa kupanda Ligi Kuu 2013 – Crystal Palace 1-0 Watford
 • Fainali ya Capital One Cup 2014 – Manchester City 3-1 Sunderland

Rekodi za kadi

 • Mechi: 349
 • Kadi za njano: 1,179
 • Kazi za njano: 57

Atkinson ana beji ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Alianza kuchezesha akiwa na miaka 16 na sasa ni miongoni mwa marefa wenye heshima kubwa kwenye Premier League.

Mwaka 1998 alianza kama mshika kibendera kabla ya kuingia rasmi kama refa wa kati katika mechi za madaraja ya chini 2002.

Michael Oliver

Tarehe ya kuzaliwa: 20/2/1985

Mji: Ashington

Alijiunga Premier League: 2010

Timu anayoshabikia: Newcastle

Mechi kubwa alizochezesha:

 • Fainali Kombe la FA 2018 – Manchester United 0-1 Chelsea
 • Fainali ya Kombe la Ligi 2016 – Liverpool 1-1 Manchester City (Liverpool walishinda kwa penalti 3-1)
 • Ngao ya Jamii 2014 – Manchester City 0-3 Arsenal

Rekodi za kadi:

 • Mechi: 203
 • Kadi za njano: 656
 • Kadi nyekundu: 28

Oliver ni miongoni mwa marefa vijana kwenye Premier League, na alianza rasmi kujihusisha na kazi hiyo akiwa na miaka 14, kipindi hicho akisimamiwa na baba yake, Clive.

Alipandishwa rasmi kuchezesha Ligi za madaraja ya chini mwaka 2007, kabla ya kupewa rasmi beji ya Fifa 2012 na 2018 kuwa mjumbe mkubwa wa Shirikisho la Ulaya (UEFA).

Jon Moss

Tarehe ya kuzaliwa: 18/10/1970

Mji: Sunderland

Alijiunga Premier League: 2011

Timu anayoshabikia: Sunderland

Mechi kubwa aliyochezesha:

 • Kombe la FA 2015- Arsenal 4-0 Aston Villa

Rekodi za kadi

 • Mechi: 173
 • Kadi za njano: 584
 • Kadi nyekundu: 25

Moss alianza kuwa mchezaji wakati akiwa mwanafunzi wa chuo kabla ya baadaye kujiunga na klabu ya mtaani kwao, Sunderland. Alianza kuwa refa wa mtaani mwaka 2005, kisha kupandishwa rasmi kwenye mechi rasmi 2010.

Andre Marriner

Tarehe ya kuzaliwa: 1/1/1971

Mji: Birmingham

Alijiunga Premier League: 2005

Timu anayoshabikia: Aston Villa

Mechi kubwa alizochezesha:

 • Fainali ya Kombe la FA 2013 – Wigan 1-0 Manchester City
 • Mchujo wa kupanda Ligi Kuu 2008 – Blackpool 3-2 Cardiff
 • Ngao ya Jamii 2010 – Manchester United 3-1 Chelsea

Rekodi ya kadi

 • Mechi: 282
 • Kadi za njano: 911
 • Kadi nyekundu: 52

Marriner alizaliwa Birmingham na kuingia kwenye urefa mwaka 2005. Alipewa beji ya FIFA 2009, lakini alipokonywa mwaka 2017

Anthony Taylor

Tarehe ya kuzaliwa: 20/10/1978

Mji: Manchester

Alijiunga Premier League: 2010

Timu anayoshabikia: Altrincham

Mechi kubwa alizochezesha

 • Fainali ya Kombe la FA 2017 – Arsenal 2-1 Chelsea
 • Fainali ya Kombe la Ligi 2015- Chelsea 2-0 Spurs
 • Mchujo wa kupanda Ligi Kuu 2018 – Fulham 1-0 Aston Villa

Rekodi ya kadi

 • Mechi: 193
 • Kadi za njano: 662
 • Kadi nyekundu: 30

Taylor aliingia rasmi kwenye urefa mwaka 2010 na miaka mitatu baadaye kupewa beji ya Fifa.

Mike Dean

Tarehe ya kuzaliwa: 2/6/1968

Mji: Wirral

Alijiunga Premier League: 2000

Timu anayoshabikia: Tranmere

Mechi kubwa alizochezesha

 • Fainali Kombe la FA 2008 – Portsmouth 1-0 Cardiff
 • Fainali Kombe la Ligi 2011 – Arsenal 1-2 Birmingham

Rekodi za kadi 

 • Mechi: 453
 • Kadi za njano: 1631
 • Kadi nyekundu: 90

Dean alianza safari ya urefa 1985, kabla hajapandishwa kuchezesha mechi rasmi za madaraja ya chini ilipofika 1997. Beji ya Fifa aliipata 2003 na miaka 10 baadaye alijiuzulu.

Craig Pawson

Tarehe ya kuzaliwa: 2/3/1979

Mji: Sheffield

Alijiunga Premier League: 2013

Timu anayoshabikia: Sheffield United

Mechi kubwa alizochezesha:

 • Ngao ya Jamii 2016 – Leicester 1-2 Manchester United
 • Nusu fainali Kombe la FA 2017 – Arsenal 2-1 Manchester City

Rekodi ya kadi

 • Mechi: 108
 • Kadi za njano: 362
 • Kadi nyekundu: 17

Refa mdogo katika ngazi kubwa ya urefa. Pawson alianza kuwa refa wa akiba kabla hajawa refa wa kati 2008. Beji yake ya Fifa alipewa mwaka 2015.

Kevin Friend

Tarehe ya kuzaliwa: 6/7/1971

Mji: Tottenham, London

Alijiunga Premier League: 2009

Timu anayoshabikia: Bristol City/Leicester

Mechi kubwa alizochezesha

 • Fainali Kombe la Ligi 2013 – Swansea 5-0 Bradford
 • Ngao ya Jamii 2012 – Chelsea 2-3 Manchester City

Rekodi ya kadi

 • Mechi: 178
 • Kadi za njano: 629
 • Kadi nyekundu: 20

Friend ni miongoni mwa marefa wenye uzoefu zaidi England, akianza rasmi kazi hiyo mwaka 1984. Mchezo wake mkubwa wa heshima alichezesha 2013, fainali ya Kombe la Ligi Swansea walipocheza dhidi ya Bradford City.

Marefa wengine wa Premier League

Lee Mason:

Alianza:  2006

Mji: Bolton

Timu anayoshabikia: Bolton.

Lee Probert

Alianza: 2007

Mji: Gloucestershire

Timu anayoshabikia: Haijulikani

Roger East:

Alianza: 2013

Mji: Wiltshire

Timu anayoshabikia: Haijulikani

 

Bobby Madeley:

Alianza: 2013

Mji: Wakefield

Timu anayoshabikia: Huddersfield.

Graham Scott

Alianza: 2015

Mji: Oxford

Timu anayoshabikia:  Swindon.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here