Home Michezo Kimataifa ERIKSEN MATUZO Mdenish mwenye rekodi ya kutwaa tuzo

ERIKSEN MATUZO Mdenish mwenye rekodi ya kutwaa tuzo

6296
0
SHARE

LONDON, ENGLAND


KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Denmark, Christian Dannemann Eriksen, alikuwa mwiba mchungu kwa timu ya Wales, akiwatungua mabao mawili michuano ya Uefa Nations League.
Ulikuwa ni mchezo wake wa 83 tangu aanze kuichezea timu ya Taifa 2010, lakini pia akifikisha jumla ya mabao 25, idadi sawa na aliyofunga akiwa na timu ya Ajax ya Uholanzi.
Eriksen, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ngazi ya klabu anakipiga katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya England, kipaji chake kilianza kuonekana akiwa na umri wa miaka 10.
Umahiri wake umemfanya kuwa tegemeo kwenye kwenye kikosi cha Spurs ya Kocha Mauricio Roberto Pochettino, ambacho kwa misimu ya karibuni kimekuwa king’ang’anizi ‘top four’ kikipata nafasi ya kushiriki UEFA.
Zifuatazo ni pointi tano za nyota huyo aliyesajiliwa na Tottenham kwa kitita cha pauni milioni 11, 2013 akitokea Ajax ya Uholanzi, mchezo wake wa kwanza kucheza ikiwa ni Septemba dhidi ya Norwich.
Mchezaji bora chipukizi 2008
Kipaji kikubwa miguuni mwake akiwa na timu ya Taifa ya Denmark ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kilimwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji bora kinda 2008.
Baada ya miaka mitatu baadaye alifanikiwa kwa mara nyingine kutwaa tuzo ya mchezaji bora kinda mwenye kipaji ngazi ya klabu yake ya Ajax, akiwa tayari amepandishwa timu ya wakubwa.

Awa lulu mara nne
Mwendelezo wa kutwaa tuzo hiyo imekuwa kama jambo la kawaida, kwani mwaka 2013 alichukua mara nne tuzo. Akiwa na timu ya Taifa ya wakubwa amechukua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka mara nne.
Mbali na 2013, aliitwaa 2014, 2015 pamoja na 2017 na kujikuta akijiwekea rekodi ya Mdenmark pekee aliyechukua tuzo hiyo mara tatu mfululizo, pamoja na mabao yake 41 aliyofunga Ligi Kuu England.
Kama wote 2017/2018
Wakati straika wa Liverpool, Mohamed Salah anatwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018/19 Ligi Kuu England, Eriksen yeye alikuwa sehemu ya kikosi bora cha msimu huo.
Kabla ya kuingia katika kikosi hicho cha wanaume 11 walioutendea haki zaidi mpira, Aprili mwaka huu alitwaa tuzo ya bao bora alilowafunga Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge.
Tottenham hawakuwa mbali
Ndani ya klabu yake hiyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora viunga hivyo mara mbili msimu wa 2013/2014 pamoja na 2016/17.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here