Home Makala Eto’o atabiri bingwa Afcon

Eto’o atabiri bingwa Afcon

734
0
SHARE

ACCRA, Ghana

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon, Samwel Eto’o, amesema bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakuwa ni timu isiyotarajiwa.

Eto’o ameviambia vyombo vya habari nchini Cameroon kwamba, anavyoangalia michuano hiyo ambayo itafanyika mwakani nchini Gabon, timu itakayotwaa ubingwa itakuwa haitarajiwi wa mtu yeyote.

“Nimeangalia karibu timu zote zikicheza kwenye mechi mbalimbali, ikiwemo kufuzu Kombe la Dunia, lakini niseme ukweli kwamba, kazi ipo kweli kweli ili kutwaa ubingwa.

“Kwa mfano nikizungumzia ubora wa timu zilizopata nafasi hiyo, naona viwango vya soka letu vinafanana.

“Kwa mazingira hayo sioni timu ambayo inaweza kusema imefanya kazi kubwa zaidi ya nyingine, ila upinzani utakuwepo mkubwa, tofauti na baadhi ya watu wanavyoitazama,” amesisitiza nyota huyo.

Michuano ya Afcon inatarajiwa kuanzia kutimua vumbi Januari mwakani, lakini baadhi ya mataifa yakiwa hayapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na historia  kutokuwa na wachezaji wenye majina makubwa duniani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here