Home Michezo Kimataifa EVRA APONDWA KILA KONA, UEFA KUTOMWACHA SALAMA

EVRA APONDWA KILA KONA, UEFA KUTOMWACHA SALAMA

731
0
SHARE

NYON, Uswisi

WAKATI wadau mbalimbali wa soka wakisubiri mitanange miwili ya kukata na shoka leo baina ya timu nne kutoka maeneo mawili ya London na Manchester, tukio la beki mkongwe wa Marseille, Patrice Evra, kumpiga teke shabiki wa timu yake nalo limetikisa vilivyo.

Evra, alijikuta akitolewa uwanjani kabla hata mchezo wa Ligi ya Europa haujaanza baina ya timu yake na Vitoria, kwa kitendo cha kumtandika shabiki huyo teke la uso.

Beki huyo wa kushoto aliyewahi kuitumikia Man United, alionekana kushindwa kuzizuia hasira zake katika mzozano na mashabiki wa kikosi chake na kuishia ‘kumfumua’ teke shabiki mmojawapo.

Na sasa Evra, 36, yuko hatarini kukutana na kibano cha Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kufuatia tukio hilo lililofanana kabisa na la mwaka 1995 ambapo Eric Cantona alimtandika teke shabiki kwenye uwanja wa Selhurst Park.

Picha hizo zilizomwonesha Evra akiruka mithili ya mcheza Kung-Fu, ziliwashtua wengi na hata magazeti mbalimbali Ulaya kumwelezea nyota huyo kuwa ametia aibu.

Gazeti la L’Equipe la Ufaransa, lilitoka na kichwa cha habari kilichosema ‘Haikubaliki’, chini yake wakiandika: “Kabla ya mechi dhidi ya Vitoria, Evra alimpiga teke shabiki wa Marseille ambaye alimtolea kauli za maudhi.”

“Huenda Evra alikuwa akiyaaga rasmi maisha ya soka la kulipwa. Inategemea lakini na uzito wa ripoti ya mwamuzi, huenda akasimamishwa kwa miezi kadhaa.”

Nalo Gazzetta dello Sport la Italia lilitoka na habari iliyoanza hivi: ‘Mpira wa miguu usoni mwa shabiki’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here