Home Habari FAILI LA WAANGOLA LANASWA JANGWANI

FAILI LA WAANGOLA LANASWA JANGWANI

402
0
SHARE

yngNa Mwandishi Wetu

YANGA imefanya umafia na kukamilisha kuwasoma wapinzani wao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) GD Sargada Esperanca ya Angola, na sasa kinachosubiriwa ni mauaji tu pale timu hizo zitakapokutana kwenye Uwanja wa Taifa Mei 7, mwaka huu.

Yanga na Sagrada Esperança kutoka Luanda Norte, Angola zinakutana katika mechi ya hatua ya 16 bora ambapo bingwa atavuka kuelekea hatua ya makundi.

Kuelekea mpambano huo, Yanga haikufanya ajizi, ilikuwa ikifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha inanasa siri za wapinzani wao hao ambapo iliweza kupenyezewa kupitia kwa winga wao wa zamani Said Maulid ‘SMG’ ambaye yuko nchini Angola.

Mmoja wa watu wa karibu wa benchi la ufundi la Yanga ameliambia DIMBA kwamba wameelezwa na SMG kwamba Esperanca si timu ya kubeza kwani inacheza soka ambalo halitabiriki.

“SMG ametuambia kwamba tusiwadharau jamaa kwani soka yao haitabiriki. Kuna wakati wanacheza soka ya taratibu na kuna wakati wanacheza soka ya kasi. Hawatabiriki ndio maana wamezitoa timu ngumu kwa hiyo na sisi tumeambiwa tuwe makini,” alisema mtoa habari.

Aliongeza kuwa, timu hiyo pia mbali na kucheza soka la nguvu na kasi ni vyema Yanga wakajiandaa na hilo, pia ni wajanja kwenye ‘figisufigisu’ za nje ya uwanja.

“Jamaa katueleza kuwa wanazo mbinu za nje ya uwanja kama kuwachelewesha uwanja wa ndege, pia
wawe makini na usafiri, chakula, kiufundi ni timu inayotumia nguvu na ina kasi.”

Baada ya kunasa taarifa hizo, Yanga imechunguza kwa makini na kugundua kuwa Esperanca inao wachezaji wawili hatari ambao ni wa kuchungwa majina yao yakiwa ni Guedes na Joka.

Ili kufuzu hatua hiyo Esperanca ilizitoa timu kama Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2, ikawang’oa Liga Desportiva de Maputo kwa mabao 2-1, kabla ya kuifurusha Vita Club Mokanda ya Jamhuri ya Congo kwa mabao 4 – 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here