Home Michezo Kimataifa Fekir aisubiri Man City kwa hamu

Fekir aisubiri Man City kwa hamu

3692
0
SHARE

LYON, Ufaransa

NAHODHA wa timu ya Lyon, , amewatoa hofu mashabiki wa klabu yake hiyo kwa kuthibitisha kwamba atakuwepo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City, utakaochezwa keshokutwa, Jumanne.

Kauli hiyo ya kiungo mshambuliaji huyo imekuja kufuatia mashabiki kuhofia pengine atashindwa kucheza kwenye mtangange huo wa Jumanne, baada ya kumshuhudia akitolewa nje kutokana na jeraha alilopata dhidi ya Saint-Etienne.

Lyon ilichuana na Saint-Etienne juzi kwenye mchezo wa Ligue 1 uliochezwa kwenye dimba la Parc Olympique Lyonnais na kufanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Lakini nyota huyo wa Ufaransa alisema: “Niko vizuri, kwa sasa najiuguza. Mchezo ulikuwa mgumu lakini muhimu tumeshinda, nitakuwepo Jumanne dhidi ya Man City.”

Bao pekee la Lyon katika mchezo huo muhimu lilifungwa na beki wa zamani wa Man City, Jason Denayer, ushindi ambao uliwapandisha Lyon hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligue 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here