Home Habari FOMESHENI MPYA YA MAUAJI SIMBA HII HAPA

FOMESHENI MPYA YA MAUAJI SIMBA HII HAPA

757
0
SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

AZAM FC wanatakiwa kujipanga sawasawa kukabiliana na safu kali ya ushambuliaji ya Simba, kwani yule Mghana Nicholas Gyan, huku pia John Bocco na Haruna Niyonzima wakiwa wameshapona majeraha yaliyokuwa yakiwakabili.

Ni juzi tu Ruvu Shooting wanatoka kupokea kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 7-0, wakati Gyan na Bocco wakiwa hawapo na sasa wawili hao wameongezeka ambapo wenye timu yao wanadhani kuwa Wanalambalamba hao watakiona cha mtema kuni.

Timu hizo zinatarajiwa kukutana Jumatano ya wiki ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kila moja ikiingia na ari kutokana na kushinda michezo yao ya ufunguzi ambapo Simba waliifunga Ruvu Shooting mabao 7-0, Azam FC wakiwafunga Ndanda FC bao 1-0.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara, amethibitisha kuwa Bocco na Niyonzima wameshapona na tayari wameanza mazoezi huku pia akidai Shomari Kapombe naye muda wowote atakuwa fiti.

Kupona kwa Bocco kunamaanisha kwamba anakwenda kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji yenye wakali kama Emmanuel Okwi, Juma Luizio pamoja na Laudit Mavugo na Gyan aliyekuwa kwao Ghana kumalizia mkataba wake.

Gyan alicheza mchezo wa Simba Day dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda, ambapo alionyesha uwezo mkubwa na baada ya mchezo huo alirejea kwao kumaliza mkataba wake na klabu ya Ebusue Dwarfs na sasa mambo yamekamilika.

Meneja kwa kikosi hicho, Dk. Cosmas Kapinga, amesema Gyan anatakiwa kuanzia Septemba mosi awe ameshajiunga na wenzake, hiyo ikimaanisha kuwa ataiwahi mechi dhidi ya Azam FC, hiyo Septemba 6.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here