Home Dondoo za Ulaya Forlan awataka Man United kumpa kazi Mourinho fasta

Forlan awataka Man United kumpa kazi Mourinho fasta

500
0
SHARE

diego forlanMANCHESTER, England

STRAIKA wa zamani wa Manchester United, Diego Forlan, ameishauri klabu hiyo kuwa kocha pekee anayeweza kuwatoa kwenye majanga waliyonayo hivi sasa ni Jose Mourinho tu na wasijidanganye kuhusu Giggs.

Kumekuwa na taarifa nyingi zinazoonyesha kuwa Mourinho anakaribia kutua Old Trafford, licha ya kuibuka kwa uvumi kuwa United wanaweza wakampa mwaka mmoja zaidi Louis van Gaal wa kumalizia mkataba wake.

Lakini pia nyota baadhi wa United kama Bryan Robson, Dwight Yorke, Andy Cole na Nemanja Vidic, wameshapendekeza kuwa Ryan Giggs akabidhiwe timu kwa kuwa anafahamu tamaduni na falsafa za klabu hiyo.

“Nafikiri kwa namna walivyo katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni, United wanahitaji kocha mwenye kiwango kama Mourinho, alisema Forlan akizungumza na mtandao wa 888.com.

Mourinho ana rekodi ya kutwaa mataji mengi katika maisha yake ya ukocha akiwa na klabu tofauti tofauti, hivyo Forlan anamtazama kama mtu sahihi wa kuibeba United na kurudi kwenye utawala wake wa kugombea mataji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here