Home Michezo Kimataifa FURAHA YA MOURINHO NI KUENDELEA KUINOA MAN UNITED

FURAHA YA MOURINHO NI KUENDELEA KUINOA MAN UNITED

5935
0
SHARE

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United anasema furaha yake ni kutimiza ndoto zake za  kuwawezesha Mashetani hao Wekundu kufanakiwa maradufu, licha ya kupitia wakati mgumu hasa siku za karibuni ikiwemo kusuasua Ligi Kuu England.

Mreno huyo mwenye mataji mawili ya Uefa, usiku wa jana alikiongoza kikosi hicho kuwavaa Juventus mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.

Mourinho aliyechukua mikoba ya Mdachi, Louis Van Gaal 2016, anaweka wazi kuwa: “Ndoto zangu zipo hapa hapa, najisikia furaha bado, nina mkataba wa muda mrefu, nafikiri mafanikio zaidi hapa Man United.”

“Nasema nina furaha kubwa kushuhudia kiwango cha juu cha wachezaji katika mechi mbili zilizopita, sitaki kuzungumzia matokeo yaliyotokea, lakini huo ubora ndio ninaouhitaji,” alisema.

Kauli hiyo ya Mourinho inakuja baada ya kupindua matokeo dhidi ya Newcastle United akitokea nyuma ya mabao 2-0 hadi dakika ya mwisho kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, kabla ya Jumamosi kulazimisha sare ya 2-2 mbele ya Chelsea.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here