SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya mashabiki wa mwanadada Vanessa Mdee kuchoshwa na ukimya wa mrembo huyo, msanii mwenzake Gift Stanford ammekingia kifua kutokana na ukimya wake.

Vanessa Mdee kwa siku za hivi karibuni amedaiwa kutotoa ngoma mpya kwa madai amekua karibu zaidi na mpenzi wake Rotimi kitu amb acho huenda kikamwondoa kwenye ubora wake kama ilivyokua awali.

Akizungumza na DIMBA,Gigy Money alisema,mashabiki hawapaswi kumuhukumu Vanessa kwa kuwa muziki hauhitaji kutumia nguvu kubwa kupata ma shabiki.

ìNadhani Vanessa angeachwa atulie kwa kuwa anajua anafanya nini, hawapaswi kuzungumzia ukimya wake kwa kuwa ni mtu anayejielewa, atulie afanye kitu kwa wakati wake,îalisema Gigy Money.

Aidha Gigy Money amefurahishwa na utulivu wa Vanessa wa sasa akiwa na mpenzi wake akiamini ni moja ya mahusiano yatakayofika mbali zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here