Home Michezo Kimataifa GILBERTO SILVA ASEMA MUDA WA WENGER KUONDOKA UMEFIKA

GILBERTO SILVA ASEMA MUDA WA WENGER KUONDOKA UMEFIKA

322
0
SHARE

LONDON, England

NYOTA wa zamani wa Arsenal, Gilberto Silva, amesema muda umefika sasa kwa kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, kufungasha virago vyake na kuondoka zake.

Silva ambaye alifanya kazi kubwa kukisaidia kikosi cha Arsenal kilichoweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England bila kupoteza mchezo msimu wa 2003/04 (Invisibles), anaamini meneja wake huyo wa zamani anazidiwa na wapinzani wanaochipukia kama Antonio Conte, Pep Guardiola na Jurgen Klopp pia na nguvu kubwa ya usajili inayotumika kwenye klabu zao.

“Ubora ule wa zamani umefikia mwisho na muda wake umefika si kwa sababu hawezi kufanya kazi yoyote, bali ni kuwa klabu nyingine zimebadili mfumo wa ufanyaji kazi kwa jinsi wanavyoendesha vitu,” alisema.

“Wenger hajabadilika sana, hajabadili pia namna ya kufanya kazi yake na si kwa sababu hataki kufanya hivyo, lakini ni ngumu kushindana na timu nyingine kutokana na kuwa timu hizo zinatumia fedha nyingi kujiendesha kila msimu mpya unapoanza.

“’Wenger ametumia miaka mingi zaidi yao (Conte, Guardiola na Klopp) Ligi Kuu England. Wao ni vijana na pia wana nguvu ya kuangalia mzunguko na vyanzo vya kushinda dhidi yake,” aliongeza Silva.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here