SHARE

NA JESSCA NANGAWE

RAPA kutoka kundi la Weusi, anayefanya vyema kwa sasa na ngoma yake mpya ya ‘Gusanisha’ George Mdeme ‘Gnako’ amesema sababu kubwa iliyopelekea kumshirikisha mpenzi wake kama Video Vixen ni ubunifu wake kwenye mavazi.

Gnako ambaye amethibitisha video hiyo kuwa katika hatua za mwisho kumalizika, alisema sio kama amepunguza gharama katika kutumia warembo wengine bali aliona mpenzi wake ana vigezo alivyovitaka.

Gusanisha ni ngoma ambayo imepokelewa kwa ukubwa wa aina yake kwa mashabiki zangu, nadhani ni lazima niitendee haki kwenye video, nilimshirikisha mpenzi wangu akakubali, nikaona anakidhi vigezo navyovitaka mimi, nikaona haina tabu acheze nafasi hiyoîalisema Gnako.

Aidha rapa huyo amesisitiza kwenye video hiyo ameongeza ujuzi wa aina yake hivyo mashabiki zake wakae mkao wa kula wataiachia hewani wakati wowote kuanza sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here