Home Burudani GOODLUCK GOZBERT ATEMA YA MOYONI

GOODLUCK GOZBERT ATEMA YA MOYONI

438
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STAA wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert, amesema kipaji cha kuimba anapita tu, kwakuwa anaamini Mungu amemfungulia kipaji kikubwa zaidi ya hicho na kusisitiza hajifichi kwenye mwavuli wa dini.

Gozbert, ambaye anatamba na kibao cha ‘Shukran’ pamoja na ‘Acha waambiane’, amesema awali hakuwa na ndoto za kuwa mwimbaji, lakini Mungu aliamua kumtumia kwa ajili ya kufikisha ujumbe na anaamini ana karama nyingine ambayo anatakiwa kuifanya.

“Natamani Mungu anitumie zaidi ya hapa, naamini nina kipaji kikubwa ndani yangu zaidi ya kumuimbia Mungu, awali sikutarajia kama ningekuwa mwimbaji na hapa najua napita tu, yapo makusudi ya Mungu ambayo bado sijafikia,” alisema Gozbert.

Aliongeza kuwa, wapo watu wanaoamini anatumia mwavuli wa dini kufanya mambo ya kidunia, lakini mwenyewe amekanusha na kusisitiza yupo kwa ajili ya kusudi la Mungu na kamwe hatishwi na watu wanavyomtazama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here