Home Michezo Kimataifa Griezmann aleta utatu mwingine wa nguvu Barca

Griezmann aleta utatu mwingine wa nguvu Barca

0
SHARE

CATALONIA, Hispania

BAADA ya Barcelona kufanikisha  usajili wa straika Mfaransa, Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid, tayari nyota huyo anapewa nafasi kubwa ya kutengeneza  safu mpya ya  watu watatu langoni kwa wapinzani.

Uwezo wake wa kutumia nafasi kufunga mabao ya kutosha La Liga na michuano mingine mikubwa unamfanya nyota  huyo  moja kwa moja kuungana na Lionel Messi pamoja na Luis Suarez.

Mbali na uwezo wake, lakini pia Kiasi kikubwa cha pesa zaidi ya pauni milioni 100 aliyonunuliwa   kinamchagiza pia kocha wa kikosi hicho, Ernesto Valverde kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza.

Uimara wa Messi na Suarez  kikosini hapo wakiwa ndo wenye idadi kubwa ya mabao unapa kipaumbele zaidi ya kucheza sambamna na nyota huyo tofauti na ilivyo kwa  Ousmane Dembele ambaye mara nyingi amekuwa kaitokea benchi pamoja na Philippe Countinho.

Awali  safu hiyo ya ushambuliaji iliyofanya vizuri sana ilikuwa ni Messi, Suarez  na Neymar Jr ikipachikwa jina  la MSN, lakini baadaye alipowasili  Dembele ilijulikana kama MSD yaani Messi , Suarez  sambamba na Dembele.

Utatu wa MSG unapewa nafasi kubwa kufunga zaidi ya mabao 100 msimu ujao kwani takwimu za msimu 2015/16 zinaonyesha  watatu hao walikuwa wamefunga mabao 132, lakini  Griezmann akiwa  nje wawili hao.

Msimu wa  2018/19  mabao( 97), 2017/18  mabao  (105), 2016/17 mabao (117), lakini msimu bora zaidi ilikuwa ni  2015/16,  ambapo  Messi  alifunga mabao  41, Suarez( 59)  na Griezmann (32 ) sawa na jumla ya mabao 132.

Rekodi kali ya mabao mengi  muunganiko wa Messi , Surez na Neymar (MSN) ilikuwa ni msimu wa 2015/16 wakiwafunga jumla ya mabao 118, Neymar akifunga mabao 31.

Wakati huo klabuni hapo inaelezwa  Philippe  Coutinho, Ousmane Dembele, Semedo  Samuel Umtiti  hawapo katika  mipango ya  kocha, Ernesto Valverde .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here