Home Michezo Kimataifa GRIEZMANN MIKONONI MWA ED WOODWARD

GRIEZMANN MIKONONI MWA ED WOODWARD

316
0
SHARE

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, ameuthibitishia mtandao wa Sky Sports kuwa majukumu yote ya usajili wa majira ya kiangazi, likiwamo dili la Antoine Griezmann, amemwachia Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa klabu hiyo, Ed Woodward.

Mourinho anataka kuwaleta wakali wanne pale Old Trafford kabla ya msimu kuanza, Griezmann akiwa ndiye staa mkubwa anayesubiriwa.

Akijibu swali aliloulizwa na makao makuu ya Sky Sports kuhusu uhamisho unaosubiriwa kwa hamu wa Griezmann, Mourinho alijibu kwamba, kila kitu kipo mikononi mwa Woodward tangu alipompa orodha ya wachezaji atakaowahitaji kwenye dirisha kubwa la usajili miezi michache iliyopita.

“Kuhusu Griezmann? Sifahamu. Hilo swali ungemuuliza Ed Woodward. Tangu Machi anajua kila ninachokihitaji,” alisema Mourinho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here