Home Michezo kitaifa GUINEA YAPATA KOCHA MPYA

GUINEA YAPATA KOCHA MPYA

4573
0
SHARE
CONAKRY, Guinea

GUINEA imemtangaza Paul Put kuwa kocha mpya wa timu ya taifa hilo, kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019, zitakazofanyika nchini Cameroon.

Put hivi karibuni alikuwa akiifundisha Kenya (Harambee Stars) kabla ya kujiuzulu kwa hiari yake nafasi hiyo baada ya kumalizika kwa mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani (Chan).

Kenya ilishindwa kushiriki baada ya Shirikisho la Soka Afrika kuinyang’anya uenyeji kwa sababu za kiusalama.

Ijumaa iliyopita, Chama cha Soka Guinea kilimtangaza kocha huyo raia wa Uholanzi,  kama kocha mkuu ikiwa ni maandalizi yake kuhakikisha inapata nafasi ya kushirki fainali hizo za Afrika.

Kwa mujibu wa GFA, kazi kubwa kwa Put ni kuhakikisha nchi hiyo inapata nafasi ya kushiriki fainali hizo huku ikitarajiwa kuanza kazi mchezo dhidi ya Mauritania ambao utakuwa wa kirafiki utakaopigwa kwenye mji wa Nouakchott, Mauritania Machi 24, mwaka huu.

Guinea ipo Kundi H pamoja na timu za Ivory Coast, Rwanda na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye harakati za kufuzu michuano hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here