SHARE

NA JESSCA NANGAWE

RAPA Gnako amefunguka kuwa mke wake Yasinta si muumini wa nyimbo zake lakini baada ya kuachia ngoma yake mpya ya ëGusanishaí imeonekana kumgusa na kueleza sababu ya kuipenda.

Gusanisha ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vyema kwa sasa sehemu mbalimbali hasa baada ya video yake kuachiwa rasmi huku ndani akiwa amemshirikisha Maua Sama.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Gnako alisema, aina yake ya kurap haijapokelewa na mke wake kwa kuwa si mpenzi wa nyimbo hizo lakini baada ya kutoa ngoma hiyo ameonekana kuipenda sana kudai mashairi yake yamebeba ujumbe mzuri ndani yake.

ìHii ni nyimbo ambayo nimetua mbinu tofauti kuhakikish inamvutia kila mtu, kwa mara ya kwanza hata mke wangu ameipenda, si mpenzi wa nyimbo za rap lakini sasa amenikubaliîalisema Gnako.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here