Home Michezo Kimataifa HAMILTON TISHIO BELGIAN GP

HAMILTON TISHIO BELGIAN GP

475
0
SHARE

BRUSSELS, Ubelgiji

BINGWA mara tatu wa mbio za magari wa Kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton, ameendelea kutamba kwa kuwabwaga mahasimu wake katika maandalizi ya mashindano ya Belgian Grand Prix mara baada ya kutumia muda wa 1:44.753.

Hamiltoni amepania kubeba taji hilo katika mashindano hayo ambayo yanatarajia kufanyika katika eneo la Spa-Francorchamps Circuit.

Mkali huyo wa Mercedes, alimwacha mbali dereva wa kampuni ya Ferrari,  Kimi Raikkonen, raia wa Finland, aliyekuwa akimfuatia kwa karibu ambaye alitumia muda wa 1:45.015, huku  dereva mwenzake wa timu ya Valtteri Bottas akishika nafasi ya tatu na kuachwa kwa sekunde 0.427.

Mjerumani Sebastian Vettel wa (Ferrari) alitupwa hadi nafasi ya tano akiwa ametumia muda wa 1:45.235, huku akiwa ameachwa kwa sekunde 0.472 na dereva wa Kampuni ya Red Bull Max Verstappen aliyeshika nafasi ya nne

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here