Home Burudani HARMORAPA ATAKA KOLABO NA MATONYA

HARMORAPA ATAKA KOLABO NA MATONYA

429
0
SHARE

NA SHARIFA MMASI,

KINDA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Athuman Omar ‘Harmorapa’, amemuomba msanii mwenzake, Shaaban Seif ‘Matonya’ kufanya naye marudio (Remix) ya wimbo wake mpya wa ‘Utamu’ unaotamba kwa sasa.

Akizungumza na DIMBA, Matonya alisema ameyapokea maombi ya Harmorapa na ameanza kuyatafakari kabla ya kufikia uamuzi sahihi.

“Nimekutana na Harmorapa na kupiga naye stori nyingi ,lakini moja ya mambo muhimu na mazuri aliyoniambia ni kutaka nifanye naye remix ya ngoma yangu mpya ya ‘Utamu’.

“Siwezi kutoa majibu moja kwa moja kama nitafanya au sitafanya, nahitaji muda mwingi wa kufikiria na kuangalia upepo wa mashabiki wangu unaelekea wapi ndiyo nifanye maamuzi ya faida kwangu na kwao,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here