Home Habari ‘Hat trick’ ya Moura yaipandisha Spurs

‘Hat trick’ ya Moura yaipandisha Spurs

1317
0
SHARE

LONDON, England       

TIMU ya Tottenham imeendeleza wimbi la ushindi, baada ya kuichapa Huddersfield Town kwa mabao 4-0, yaliyofungwa na Victor Wanyama na Lucas Moura, aliyefunga mara tatu.

Mchezo huo ulichezwa mapema hapo jana na ushindi huo unawafanya Tottenham kurudi mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Baada ya ushindi huo, Moura alisema kuwa anafurahi kupewa nafasi na kocha wake, Mauricio Pochettino, huku akiwapongeza wachezaji wenzake kwa ushirikiano wanaompa wakati wote.

“Nafurahi kocha amenipa nafasi na mimi kufanya kazi yangu, lakini niwashukuru wachezaji wenzangu kutokana kwa ushirikiano wao mkubwa,” alisema winga huyo raia wa Brazil.

Moura alijiunga na Tottenham katika dirisha la Januari mwaka jana, lakini amekuwa akiingia na kutoka kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kiwango chake kushuka na kupanda.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here