Home Habari HATA LEO MINZIRO ANAWEZA KUTUA YANGA

HATA LEO MINZIRO ANAWEZA KUTUA YANGA

499
0
SHARE

NA WINFRIDA MTOI


BAADA ya kutojua hatima ya kibarua chake na Singida United, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Fred Felix Minziro, amesema Yanga wakielewana kwenye masuala ya maslahi yupo tayari kutua kikosi hicho kama Kocha Msaidizi.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Minziro alisema iwapo Yanga wataonyesha nia ya dhati, yupo tayari kujiunga na kukosi hicho, kinachonolewa na George Lwandamina, kuchukua mikoba ya Juma Mwambusi.

“Mimi ni kocha na kazi yangu kufundisha, kuna ofa nimezipata, nawasikilizia Singida wiki hii, nikiona bado hawakubaliani nitaamua kuachana nao ili nikafanyie kazi ofa zilizopo mezani kwa sasa,” alisema.

Timu ambazo zimeonyesha nia ya kumtaka Minziro ni Majimaji, KMC ya Kinondoni na Tanzania Prisons. Minziro, ambaye ni nyota wa zamani wa Yanga, ameshawahi kuifundisha timu hiyo kama kocha msaidizi kwa nyakati tofauti, hivyo kama atajiunga na mabingwa hao mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara haitakuwa mara ya kwanza.

Kocha huyo ndiye aliyeipandisha Singida na nafasi yake kuchukuliwa na Hans van der Pluijm, raia wa Uholanzi, ambapo Minziro akapewa jukumu la kuwa Kocha Msaidizi, ingawa hivi sasa bado hawajaweza kumpa mkataba mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here