Home Habari HATIMA YA BLAGNOON KUJULIKANA LEO

HATIMA YA BLAGNOON KUJULIKANA LEO

1273
0
SHARE

NA SAADA SALIM,

DAKTARI wa timu ya Simba, Yassin Gembe, amesema hatima ya straika wao, Fredrick Blagnoon kukaa nje kwa muda gani itajulikana leo, baada ya kufanyiwa vipimo vya kina.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, daktari huyo alisema baada ya vipimo na uchunguzi wa mchezaji huyo, leo atatoa majibu kwa kiasi gani alichoumia.

Alisema baada ya vipimo hivyo na kupatikana kwa majibu hayo itajulikana atakuwa nje kwa muda gani au kuruhusiwa kucheza kulingana na jinsi alivyoumia.

Blagnoon aliumia nyama za paja katika mechi na Ndanda FC, iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Blagnoon alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu kuisaidia timu yake kufanya vizuri ambapo alicheza michezo 13, huku akikosa michezo miwili kwa sababu ya kupata majeraha katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here