SHARE

LONDON, England

FRANK Lampard anaendelea kutamba baada ya kushinda mchezo wa sita mfululizo wa Ligi Kuu England akiwa na kikosi chake cha Chelsea, wakitoa kipigo cha mabao 2-0 kwa Crystal Palace.

Chelsea ambao waliuanza kwa kasi kubwa mchezo huo, walikosa mabao ya wazi kupitia kwa Christian Pulisic, Willian na Tammy Abraham na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike bila kufungana.

Iliwachukua dakika saba baada ya kipindi cha pili kuanza, Chelsea kufunga bao la kuongoza kupitia kwa straika wao Abraham ambaye alipokea pasi ya kisigino kutoka kwa Willian.

Dakika ya 79 walitanua wigo wa ushindi kwa kuongeza bao la pili kupitia kwa Pulisic aliyefunga kwa kichwa baada ya mabeki wa Crystal Palace kushindwa kuokoa mpira.

Baada ya mchezo huo wa mapema kumalizika, Chelsea walisogea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, kabla ya mechi zingine kuchezwa. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here