Home Funguka/Mapenzi HAYA NI MAAMUZI SAHIHI YA MWANAUME

HAYA NI MAAMUZI SAHIHI YA MWANAUME

4184
0
SHARE

NI somo tuliloanza nalo wiki iliyopita, tukiangalia kwa undani namna mwanamke anavyokuwa katika wakati mgumu kutokana na maamuziyaliyopo ndani ya mwanaume.

Nimeshaeleza mengi wiki iliyopita, sasa tuendelee na sehemu ya pili ya mada yetu nikiamini kuna mambo utajifunza…

SUALA LA MIMBA

Kupata mimba kabla na nje ya ndoa ni tatizo. Ni jambo moja linalowahusu watu wawili lakini likiwa ndani ya uamuzi wa mwanaumee. Mimba si bahati mbaya. Wanawake wanajua hili vizuri sana.

Wakati mwingine, wapenzi wanaweza kuwa wamepima ukimwi na hivyo wana uhuru wa kuamua kukutana kwa kutumia kinga au lah, lakini bado kuna suala la mimba ambalo linaweza kumgharimu mwanamke huyo.

Ukiacha hilo, inatokea mwanaume anamlazimisha mwanamke abebe mimba kwanza (eti) ndiyo anapeleka barua ya posa kwao. Inawezekana mwanaume huyo ana lengo hilo, lakini kwa nini alazimishe iwe kabla ya ndoa?

Kwa sababu sasa wanawake wengi huwa wanaacha nguvu yao ya kufikiri, wanajikuta wameingia mkenge! Mwisho jamaa anaingia mitini, mwanamke anabaki na mtoto wake.

Kwa nini uache hili litokee? Kwani hujui namna ya kujikinga na mimba? Ukiachana na kinga, kuna hata njia rahisi ya kuhesabu mzunguko wa mwezi, pia hujui?

Yapo mengi ya kujifunza, naamini yatabadilisha mtazamo wa wanawake wengi ambao wanalia wakiwa ndani ya tatizo lililopo kwenye mikono yao wenyewe.

KUINGILIA UHUSIANO

Wanaume walio wengi, wakishajua kwamba mwanamke fulani ana mwanaume wake ni vigumu sana kuwataka kimapenzi (hasa kama ana malengo naye), ni tofauti na mwanamke ambaye hata kama atagundua kwamba mwanaume fulani ana mtu wake, anaweza kuingilia uhusiano huo.

Zipo sababu kadhaa zinazosababisha hilo litokee, kuna mwingine anaweza kuamini (eti) yeye ni bora kuliko mwanamke aliyenaye na kwamba (pengine) anaweza kumbadilisha mwanaume huyo mawazo ili yeye amchukue jumla!

Huu ni uvivu wa kufikiri. Kama ana wake, halafu akakutaka na wewe ili iweje? Anashindwaje kukuacha hata wewe baadaye na kuchukua mwingine? Ni mambo ambayo yanawezekana. Aina ya wanawake ninayoizungumzia hapa, hawana hofu juu ya jambo hili – wanajaribu bahati zao.

Lipo kundi lingine, hili ni lile la wale ambao wanaamini kuolewa ni bahati. Kwa msingi huo, kama wametoswa na wanaume wengi, huamua kuingia kwa mwanaume yeyote kwa lengo la kujitoa nuksi (kwa wanavyoamini wenyewe).

Achana na fikra hizo. Ni nani aliyekuganganya kwamba una nuksi?

KUACHWA

Tatizo jingine linalowasumbua wengi ni kuachwa. Mwanamke huwa hajui chochote kuhusu hatma yake na mpenzi wake. Muda wowote jamaa anaweza kusema: “Mimi na wewe baasi.” Ikawa hivyo kweli.

Mara chache imetokea mwanamke naye kuamua kumuacha mwanaume au kutengeneza mazingira ya kujifukuzisha, hii hutokea mara chache sana. Mara nyingi, mwanamke hujikuta tu akiambiwa uhusiano umefikia mwisho.

Inawezekana dalili zilikuwa wazi tangu mapema, lakini kwa sababu hakupata muda wa kutafakari hilo kwa makini tangu mapema, basi hujikuta katika wakati mgumu baada ya mwanaume kuamua kusitisha uhusiano.

Wiki ijayo, mada yetu itaendelea, USIKOSE!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here