Home Habari Hazard awataka Real Madrid kufanya kweli 

Hazard awataka Real Madrid kufanya kweli 

1472
0
SHARE

MADRID, Hispania

MAMBO ni mengi lakini muda ni mchache, vigogo wa Hispania, Real Madrid wameanza chokochoko tena kwa winga wa Chelsea, Eden Hazard, baada ya kuamini kuwa staa huyo wa Ubelgiji anaweza kujiunga nao mwishoni mwa msimu huu.

Real Madrid wameweka dau la pauni milioni 100 mezani kwa Hazard ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa huku maongezi ya kumwongezea yakikwama mara kadhaa.

Mtandao wa Sky Sports nchini England ulitoboa kuwa Hazard hayupo tayari kubaki Chelsea kwa msimu ujao lakini klabu hiyo haiwezi kukubali kitita hicho cha pauni milioni 100.

Pia, Real Madrid wanahusishwa kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa Hazard mwenyewe amekuwa akijaribu kuwasiliana na wakala wake ili kufanya dili hilo likamilike mwishoni mwa msimu huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here