Home Michezo kitaifa Hazard awekwa daraja moja na Ronaldo

Hazard awekwa daraja moja na Ronaldo

429
0
SHARE
Eden Hazard

LONDON, England

GWIJI wa Chelsea, Pat Nevin, amemtazama kwa makini Eden Hazard na kujiridhisha kuwa kwa sasa winga huyo yuko daraja moja na nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.

Winga huyu wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu na kuwafanya mashabiki wa Chelsea kusahau machungu yao ya msimu uliopita.

Mpaka sasa Hazard amefunga mabao 7 kwenye mechi 11 alizocheza, huku kiwango alichokionesha kwenye mchezo dhidi ya Everton kikitajwa kuwa bora msimu huu.

“Nafikiri kwa aliyemfuatilia kwenye pambano dhidi ya Everton atakuwa ameona namna Eden Hazard alivyoimarika zaidi, yuko kwenye kiwango bora sawa na kina Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.

“Diego Costa yuko vyema sana, David Luiz ameituliza ngome ya ulinzi, kwa sasa ni kama kikosi cha wachezaji 11 wa dunia wanacheza pamoja kwenye kikosi cha Chelsea.

“Kila mchezaji anatimiza majukumu yake ipasavyo, Thibaut Courtois ametulia pia, nafikiri mazungumzo yake na Conte yalikuwa mazuri kwa pande zote mbili.

Lakini pamoja na maneno haya ya Nevin, nyota huyu wa zamani wa Chelsea alishindwa kuipa nafasi ya moja kwa moja klabu hiyo kubeba taji msimu huu.

“Lakini maneno haya simaanishi kwamba Chelsea watabeba kombe kirahisi, najua wana timu ya kuleta changamoto, japo sina hakika kama wataendelea na moto huu mpaka Mei, mwakani,” aliongeza.

” Man City, Liverpool na Arsenal wako vizuri pia na wana nafasi nzuri ya kubeba taji kama ilivyo kwa Chelsea, bado mbio za ubingwa zipo wazi.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here