SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MKALI kutoka kiwanda cha Bongofleva Nurdin Bilal maarufu ëShettaí amesema tofauti na kipaji chake cha muziki pia anafanya vitu vingi vinavyomuingizia kipato ikiwemo biashara ya kuuza chips.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Shetta alisema, anafahamu fika kazi ya muziki ina zama zake na amekua akiumiza kichwa usiku na mchana ili aweze kuendana na kasi ya maisha hivyo ameamua kujiongeza kwa kufanya shughuli nyingine.

Unajua kuna watu wanajiuliza Shetta anapata wapi pesa wakati kwenye muziki haonekani sana, ni wazi tu kijana yoyote hapaswi kutegemea kitu kimoja anapaswa kuumiza kichwa ili ajue jinsi ya kuishi mjini, watu wengi hawajui lakini mimi nauza chipsi vumbi mtaani kwangu Kunduchiîalisema Shetta.

Hata hivyo staa huyo aliyewahi kuvuma sana na nyimbo zake kama ëShikoroboí, ëHatufananií amesema yupo mbioni kukamilisha mjengo wake uliopo Madale na wakati wowote atahamia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here