SHARE


NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongomovie Hemed Suleiman maarufu kama Hemed PHD amefunguka mipango yake ya kutaka kuoa na kusisitiza kwa sasa hafikiriii hivyo labda akiwa na miaka isiyopungua 45.

Akizungumza na DIMBA, Hemed alisema, anafahamu changamoto za ndoa zilivyo hivyo kwa sasa haoni kama anahitaji kuingia na badala yake amejikita zaidi kwenye masuala ya kazi.

“Natambua umri wangu wa kuoa umefika, lakini ni jambo ambalo kwa sasa halina nafasi hata kidogo, labda nikiwa na miaka 45, nitatafuta mzee mwenzangu kisha tuunganishe familia”alisema Hemed.

Aidha alisema licha ya kujihusisha na mahusiano tofauti lakini haja wahi kujutia kupata watoto wa nje ya ndoa na ameendelea kuwa baba bora kila siku.

Kwa sasa staa huyo ameendelea kufanya vyema kwenye kiwanda cha Bongomovie huku akitarajia kuachia kazi yake mpya wakati wowote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here