Home Makala Teknolojia ilivyobadilisha maisha ya Oscar Pistorius

Teknolojia ilivyobadilisha maisha ya Oscar Pistorius

655
0
SHARE

NA FARAJA MASINDE,

MMESIKIKA! Hii ni baada ya maombi yenu ya kuomba safu ya SportTeknolojia iongezwe uwanja ikiwezekana kuwa ukurasa mzima. Hicho ndicho kinachofanyika kuanzia leo kwenye safu hii inayopatikana kwenye gazeti la DIMBA peke yake kila Jumatano.

Hapa unapata wasaa wa kufahamu, magari ya mastaa hawa, nyumba, simu utajiri wao na vingine vyote wanavyomiliki yakiwamo mahusiano yao pia, lakini pia  mikasa ya kimaisha ambayo imewahi kuwakuta au imewakuta wachezaji hawa.

Leo tunamwangazia mwanariadha ambaye kwa sasa yuko gerezani akitumikia kifungo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake na mwanamitindo wa Afrika Kusini, Reeva Steenkamp.

Pistorius aliidhihirishia dunia kuwa ulemavu si kigezo chakumzuia mtu  kutimiza ndoto zake kwenye maisha haya yaliyojawa na fursa tele zikichagizwa na teknolojia.

Licha ya kwamba Pistorius alikatwa miguu baada ya kuzaliwa na matatizo lakini haikuwa kikwazo kwa yeye kuishangaza dunia katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini London, 2012.

Ni michuano hiyo ndiyo iliyomwezesha Oscar kukusanya takribani medali 12 na hivyo kujikuta akipamba majarida mbalimbali ya michezo duniani ikiwemo jarida la Times.

Historia ya Oscar Pistorius

Oscar ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto watatu wa Sheila Pistorius na Henke, ambapo alizaliwa Novemba 22, 1986 katika jimbo la Transvaal nchini Afrika Kusini. Hata hivyo, akiwa mtoto alikumbwa na ugonjwa wa ‘Fibular Hemimelia’, ambao ni nadra sana kuwapata watoto na hivyo miguu yake yote ililazimika kukatwa.

Hata hivyo, licha ya kukatwa miguu haikuwa kigezo cha yeye kukosa elimu kwani alipata elimu katika shule ya msingi Constantia Kloof, kisha baadaye alijiunga na shule ya sekondari ya wavulana ya Pretoria.

Pia wakati akisoma katika shule ya Pretoria alikuwa akicheza mchezo la raga lakini pia alikuwa akijaribu kucheza, tenisi kwa kipindi hicho mpaka pale aliposhauriwa kukaa mbali na michezo hiyo mara baada ya kujiumiza vibaya akiwa mchezoni mwaka 2003.

Mapema mwaka 2004, Oscar alikutana na makocha wawili ambao ni Ampie Louw na Francois Van Der Watt ambao hawa wote walimtia moyo kuanza kujaribu mchezo wa riadha.

Kocha, Van der Watt alianza kwa kumsaidia kupata miguu ya bandia kwa ajili ya kumsaidia kukimbia ambayo ilimkaa vilivyo na hivyo kuanza taratibu kujikita kwenye mchezo huu wa riadha.

Ni mwaka huo huo ndio alioshiriki katika michuano ya Paralympics katika majira ya joto ya mwaka 2004 ambapo alimaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za mita 100.

Mwaka 2015 jina la Oscar lilizidi kukua mara baada ya kuibuka kinara katika michuano ya Kombe la Dunia ya Paralympic iliyofanyika Afrika Kusini, katika michuano hiyo aliyoshiriki kama mtu mwenye miguu kamili, Oscar alitumia sekunde 47.34 kukimbia mita 400.

Elimu haina mwisho! Ndio mwaka 2006 Oscar alirudi shule kuchukua shahada ya usimamizi wa biashara katika Chuo Kikuu cha Pretoria.

Utajiri

Awali kabla ya Nike kusitisha mkataba wake, Oscar alikuwa ana utajiri unaokadiriwa kufikia randi milioni 17, hii ikihusisha dili la za makampuni kama, Nike, Oakley, kampuni ya mawasiliano ya Uingereza BT na pafyumu  ya Thierry Mugler.

Tuzo

Mwaka 2007 alitunikiwa tuzo ya heshima kama mwanamichezo bora wa mwaka aliyotunukiwa na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC.

Mwaka 2012 alitunukiwa tuzo ya heshima ya Laureus World Sports kwa wanamichezo wenye ulemavu ambapo Oscar alikuwa ni miongoni mwa wanamichezo 100 miongoni mwa watu wenye ushawishi duniani katika sula la michezo ambayo pia ilichapishwa katika Jarida la TIME.

Maisha binafsi

Licha ya kuwa Oscar amehukumiwa kwenda jela lakini amekuwa ni kati ya wanaotumia vipaji vyao vizuri kuingiza mkwanja mrefu kwani ana mikataba na kampuni za Nike na Oakley, lakini pia ana pafyumu yake inayoitwa A.

Pia amewahi kutengeneza filamu yake inayoitwa Thierry Mugler, mwaka 2008 alizindua jarida nchini Italia ambalo alilipa jina la Dream Runner,  ambapo linalofuata litakuwa ni la Kiingereza.

Pistorius alikumbwa na hatia ya kwenda jela mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva kwa kumpiga risasi mnamo Februari 19, 2013.

Ilidaiwa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa na lengo la kumfanyia ‘sapraizi’ mwanariadha huyo lakini Oscar alimfyatulia risasi kwa kudhani kuwa alikuwa ni jambazi.

Alilazimika kukatwa miguu chini ya goti, umaarufu wake ulitokana na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa. Kwenye mashindano ya London kwa wasio na miguu alishika nafasi ya kwanza.

Oscar Leonard Carl Pistorius, wakati anakatwa miguu wazazi wake walitalakiana  akiwa na umri wa miaka sita hali iliyofanya uhusiano baina yake na baba yake mzazi kutetereka.

Mama yake na Oscar, alifariki dunia na kumwacha akiwa na umri wa miaka 15 kutokana na matatizo ya utumiaji wa dawa za kulevya.

Baada ya kuondolewa kwa miguu hiyo aliwekewa mingine ya bandia ambayo baadaye alifanikiwa kuitumia kutembea kwa mafanikio makubwa, hata hivyo ulemavu wake wa miguu ni kama ulipunguza mafanikio yake kwenye michezo.

vifaa vya nike kwaajili ya miguu
vifaa vya nike kwaajili ya miguu

Nike wakatisha mkataba

Kwa taarifa yako tu fahamu kuwa mara baada ya Oscar kukumbwa na balaa la kuua bila kukusudia jamaa hawa walivunja mkataba.

Mkataba huo ambao awali waliingia mwaka 2012 mara baada ya Oscar kufanya vyema kwenye Olimpiki, ulikuwa ukihusisha vifaa vya kiteknolojia ambavyo humsaidia kukimbia aina ya carbon fiber blade.

Awali Nike walisema kuwa vifaa hivyo vilikuwa vimetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kiasi cha kumfanya akimbie kama aliye na miguu, huku wakisisitiza kuwa isingekuwa rahisi kwa Oscar kupata maumivu iwapo angeanguka.

Hata hivyo, mara baada ya Oscar kukabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia, Nike kupitia kwa msemaji wao, KeJuan Wilkins, walithibitisha kuvunja mkataba na mwanariadha huyo kwa madai kuwa kitendo hicho cha Oscar kingechangia kushusha umaarufu wa bidhaa za kampuni hiyo duniani.

Kampuni ya Nike walitumia dola milioni 800 kumlipa Oscar ambaye alitumia kiasi hicho kujisomesha kwenye taaluma yake ya utawala wa biashara, ambapo kila msimu alikuwa akikunja dola milioni mbili kutoka Nike.

Hata hivyo, Nike imekuwa na utaratibu huo wa kuvunja mikataba na watu wanaoingia nao makubaliano na hii imekuwa ikitokea pale tu mtu huyo anapokumbwa na kashfa.

Usafiri

Ulemavu wa miguu haujawa kigezo kwa Oscar kumiliki usafiri, ichukue hii kuwa Oscar anamiliki usafiri aina ya McLaren supercar ambayo aliinunua kwa Rand milioni 5 za Afrika Kusini gari ambalo alinunua kama zawadi ya Krismasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here