Home Burudani Herieth Paul anatesa tu Victoria Secret

Herieth Paul anatesa tu Victoria Secret

3705
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MWANAMITINDO Mtanzania, Herieth Paul, amefanikiwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kupata nafasi ya kutembea kwenye jukwaa la maonyesho ya Victoria Secret sambamba na mastaa wakubwa duniani.

Onyesho hilo lililofanyika juzi nchini Marekani, mwanamitindo huyo aliungana na wanamitindo maarufu duniani kama Kendall Jenner, Adrana Lima, Behati, Prinsloo, Gigi, Bella, Winner Harlow na wengine wengi.

Heriet Paul amepata mafanikio makubwa kupitia maonyesho hayo ikiwa ni pamoja na kununua nyumba nchini Marekani na kwa sasa makazi yake yapo nchini humo.

Hii ni mara ya tatu kwa mrembo huyo kushiriki maonyesho makubwa kama hayo kwa mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here