SHARE

MANCHESTER, England                          

STAA wa Manchester United, Ander Herrera, amekiri kuwa mwenendo wao wa kushangaza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu unachagizwa na historia ya klabu ya Chelsea.

Man Utd ilifanya maajabu kwa kuing’oa PSG katika hatua ya 16 Bora, ambapo iligeuza matokeo ya kufungwa 2-0 nyumbani, kabla ya kushinda 3-1 ugenini.

Baada ya ushindi huo wa kihistoria, vijana hao wa kocha Ole Gunnar Solskjaer wamepangiwa kucheza dhidi ya Barcelona katika hatua ya robo fainali, lakini bado klabu hiyo ina imani ya kuwatoa jasho wababe hao.

Herrera alisema kuwa, Man Utd wanatumia historia ya Chelsea ilipotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2012 na kuwashangaza wale ambao walikuwa hawaiamini timu hiyo iliyokuwa chini ya kocha, Roberto Di Matteo.

“Hatupo kwenye mashindano yoyote England, kwenye Ligi Kuu tunaisaka nafasi ya tatu, lakini bado tuna imani na Ligi ya Mabingwa Ulaya,” alisema Herrera.

“Tukikumbuka jinsi Chelsea ya Di Matteo ilivyokosa wa kuwaamini na ikachukua ubingwa mwaka 2012, ndivyo tunavyozidi kusonga mbele,” aliongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here