SHARE

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

KIPIGO cha mabao 2-0 walichokipata timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars ‘ kutoka kwa Senegal katika mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) kimezua zogo bungeni ambapo Wabunge wameitaka Serikali kutenga bajeti kwa ajili ya timu hiyo.

Pia wamehoji ni kwanini Waziri wa Habari, Utamaduni na Sanaa na Michezo Dkt Harrsion Mwakyembe na Naibu wake Julina Shonza wapo nchini wakati Stars ikiwa inaendelea na michezo yake nchini Misri.

Zogo hilo lilitokea jana bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu,ambapo alisimama Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni,na Mbunge wa Rombo Joseph Selasini (Chadema) na kuomba mwongozo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambapo alitaka apewe majibu ni kwanini Waziri na Naibu wake wa Wizara hiyo wapo nchini.

Timu ya Taifa inaibeba nchi na kama ulivyokuwa kule Misri (Spika Job Ndugai) viongozi mbalimbali wapo lakini timu yetu tunamuona Waziri wa Michezo na Naibu wake yupo katika hali ya kawaida kisaikolojia sio sawa.

Naomba mwongozo wako, ni kwanini Mawaziri wa Michezo hawapo Cairo vile vile nikupongeze wewe kwa kuonesha mfano kuhakikisha timu ya taifa inafanya vizuri,îaliuliza

Naye,Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) alipopewa nafasi na Spika alisema: ìNilitaka kuzunguzia jambo hilo hilo kwa kweli linaumiza sana.

Kutokana na miongozo hiyo, Spika Ndugai alimwomba Mwakyembe ajibu ambapo alisema kutokana na timu ya Taifa kutokuwa na bajeti hivi karibuni aliandaa harambee ya kuichangia timu hiyo iliyoongozwa na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan.

Kuhusu ushiriki wetu tulikuwa hatuna bajeti unaweza kufikiria mwaka jana tu ningeomba bajeti ningeonekana kichaa kwanza tumeingia huko ndio maana uliniona na Makamu wa Rais kwa kuitisha harambee kuhakikisha timu yetu isiadhirikike

Sio kwamba timu ya Taifa, haikuwa na pesa ilikuwepo ya posho ya kambi ya kawaida ilikuwepo lakini huu ni ushindani mkubwa.

Alisema kila kinachopatikana kwa sasa kinapelekwa moja kwa moja kwa wachezaji 23 walioko nchini Misri.

Ndio maana sasa hivi kinachopatikana kinapatiwa wachezaji wetu 23 na kuingizwa katika Akaunti zao,îalisema Mwakyembe.

Kuhusu uwezo wa kocha wa Stars Emanuel Amunike,Mwakyembe alisema kuna maneno mengi yanasemwa lakini kunatakiwa kuwe na mjadala mpana baada ya kukamilika kwa michuano ili wasiwakatishe tamaa wachezaji.

ADAI WACHEZAJI WA KIGENI WANAUA SOKA LA BONGO

Alisema kinachoiumiza timu ya Taifa ëTaifa Starsí ni wachezaji wa kigeni kuwa wengi katika timu za Simba na Yanga.

ìIla kuna kitu kimoja Watanzania lazima tukiangalie miaka miwili iliyopita uongozi wa TFF ulibadilisha kanuni ili wachezaji kutoka nje zaidi ya watano wakawa kumi na wote wanaweza kucheza na kazi yetu kuvunja matawi kushangilia kwamba tumeshinda hilo nalo linahitaji mjadala.

Hali ilibadilika mara baada ya Mwakyembe kudai kwamba timu za Simba na Yanga zinategemea wachezaji wa viungo kutoka nje ya Nchi.

Timu zetu kubwa za Simba na Yanga ambazo ndizo zinazozalisha wachezaji zinategemea wachezaji wa nje kwa ajili ya Mildfield,îalisema Mwakyembe huku Wabunge wakipasa sauti kutokubalina na jambo hilo.

Kutokana na majibu hayo Wabunge walianza kupaza sauti kwamba anachosema Waziri Mwakyembe sio kweli huku wakihoji ni kwanini hakwenda Misri.

Ambapo Spika aliwatuliza : ìWaheshimiwa Wabunge tusikilizane tumpe nafasi Mheshimiwa Waziri amalizie.

Alipoendelea Mwakyembe alisema kwenda kwake Misri sio jambo la msingi sana.

Taifa letu liliwakilishwa na mmoja ya viongozi wetu waandamizi Spika wa Bunge.Na mimi ndio maana nikaona niwakilishwe na ujumbe kutoka CAF na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) mchango wake ulikuwa mkubwa kuliko hata mimi na wewe ulikuwepo uliona,îalisema.

HALI YABADILIKA

Wakati akiendelea kuchangia alisimama Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga (Chadema) ambapo aliomba kumpata taarifa Waziri Mwakyembe ambapo Spika Ndugai alimruhusu.

Kiwanga alisema hali ya kambi ya timu ya Taifa haikuwa nzuri ambapo alidai kwamba bila ya juhudi za watu binafsi hali ingekuwa mbaya zaidi na kwamba hakukuwa hata na bendera za Taifa.

Naomba kumpa taarifa mzungumzaji ambaye ni Waziri wa Michezo kule ingekuwa bila ya jitihada za watu binafsi, hakuna bendera Mheshimiwa Spika hakuna chochote cha uhamasishaji na yeye ndio Waziri wa Michezo hali ni mbaya mno, tukijtofautosha na mataifa mengine.

Naomba kumpa taarifa pamoja na kwamba Mhimili wa Bunge ulikwenda lakini yeye alitakiwa kusaidia shamrashamra ili Spika wetu upambwe,îalisema Kiwanga.

Mara baada ya taarifa hiyo,Mwakyembe aliendelea kwa kusema : ìwenzetu wa upande wa pili wanisikilize basi wakati naongeaî

Spika aliingilia kati kwa kuwataka Wabunge kumsikiliza Mwakyembe : ìNaomba tuwe na utulivu jamani,î

Lakini wabunge waliendelea kupata sauti wakitaka wapewe majibu.

SPIKA ATAKA MWAKYEMBE AENDE MISRI

Mara baada ya kuona utulivu umepotea Spika Ndugai alisimama na kumwomba Waziri Mkuu asimamie ili Waziri Mwakyembe aende nchini Misri kwa ajili ya kuangalia kambi ya timu ya Taifa ëTaifa Starsí

Nikuombe Waziri Mkuu vyovyote inavyokuwa kama Waziri wa michezo anaendelea kuwepo hapa haitoi picha nzuri.Tumsaidie Waziri wetu yale ya hapa nchini tuyafanye na yeye atoke aende Afcon hili jambo ni la kitaifa ni jambo kubwa mno.Na Wabunge wanaondoka kesho (leo) wakienda peke yao wakirudi peke yao halitoi picha nzuri,îalisema.

ALIA NA BAJETI

Kuhusiana na bajeti ya kwa ajili ya timu ya Taifa,Spika Ndugai alisema kuna haja ya bajeti zijazo jambo hilo liangaliwe.

Waziri wa fedha hili jambo hili tulikwambia wakati wa Bajeti wakati tunaangalia namna ya kumaliza hii miezi mitatu tulimwambia Waziri si mnakumbuka hakuna fedha kwa ajili ya timu ya Taifa?

Wakajibu kwamba fedha ipo lakini ni za under 17 sio za National team lakini pakawa na tungeweza kurekebisha hili,wakati mwingine Waziri wa Michezo hawezi kusema kila kitu.

Kama safari ijayo tutakuwa tumefuzu timu za Taifa ni timu za Serikali mliangalie haliwezi likawa jambo la kitaifa halafu hakuna serikali kwahiyo ni lazima tujue wadau, wapambe wanaunga mkono lakini Serikali ndio inatakiwa ishike bango,îalisema.

AMUNIKE

Kuhusiana na Kocha wa Stars Emanuel Amunike,Spika alichombeza kwa kusema : ìBabati nzuri Waziri Mkuu ni mwanamichezo na ni kocha anatamani hata angekuwa kule aifundishe Amunike wa nini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here