Home Burudani Hussein Jumbe arudi jukwaani leo

Hussein Jumbe arudi jukwaani leo

345
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi nchini, Hussein Jumbe, anarudi upya jukwaani leo baada ya mwezi mzima wa kuumwa hoi akiwa kitandani na kusababisha kuzushiwa kifo.

Jumbe atapanda jukwaani leo akiwa na bendi yake Talent, katika onyesho maalumu litakalofanyika katika ukumbi wa Kisuma, Tandika Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam.

Nguli huyo wa muziki wa dansi nchini kwa takribani mwezi na nusu alikuwa yuko hoi kitandani akisumbuliwa na maradhi ya mifupa na sukari kabla ya kupata nafuu hivi karibuni.

Jumbe ameliambia DIMBA Jumatano, kuwa anamshukuru Mungu kwa sasa afya yake imeimarika kiasi cha kufanikiwa kunyanyuka kitandani na leo akitaraji kuwapa burudani mashabiki wake waliomkosa kwa muda mrefu.

Alisema, atapanda jukwaani akiwa na zawadi ya nyimbo mbili mpya ambazo alitunga akiwa yu hoi kitandani, wa kwanza ukiwa ni ‘Kipima joto’ na ‘Fumbo la Matumaini’ ambazo zote zinaelezea matukio yake ya kuugua na vilevile kuwashukuru wadau wa muziki, hususan wapenzi wake waliojitokeza kumsaidia kwa hali na mali katika kipindi cha ugonjwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here