SHARE

NA MWAMVITA MTANDA

INAELEKEA soka la Tanzania linawavutia makocha wengi na kutamani kuja kufanya kazi nchini, mmoja wapo ni bosi wa As Vital ya DR Congo, Frolent Ibenge, ambaye ameweka wazi kuwa endapo Yanga au Simba watamuhitaji yupo tayari kwani anachoangalia zaidi kwake ni maslahi yake.

Ikiwa ni muda mfupi tangu kutimuliwa kwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, Simba nako zinasambaa taarifa kwamba huenda nao wakaachana na kocha wao Mbelgiji Patrick Aussems.

Kufuatia sintofahamu hizo, makocha mbalimbali wanaozijua timu hizi kongwe za Tanzania wameonyesha nia ya kutaka kuja kujaribu bahati ya kuzinoa, endapo mambo yatakwenda sawa.

Akizungumza kutoka na DIMBA kutoka Kinshasa, Ibenge alisema, anatambua ubora wa makocha wote hao, ikiwemo Aussems ambaye anadai alisoma nae kwenye mafunzo ya ukocha miaka kadhaa nchini Ufaransa na Zahera wanaekutana mara kwa mara ndani ya timu ya Taifa ya Congo.

Alisema kufahamiana kwao hakuwezi kumzuia kurithi nafasi zao kwani kila mmoja anatafuta mkate wake wa kila siku na pia anafahamu umaarufu wa timu hizo zenye mashabiki wengi.

“Bado nina mkataba na As Vita, lakini Kama watakuwa wananihitaji na kukubaliana ninachotaka, niko tayari muda wowote kufanya kazi kwao,îalisema Ibenge.

Ibenge ambaye ni raia wa Zambia ana misimu mitatu sasa ndani ya kikosi cha As Vital, pia ameshawahi kufundisha timu zaidi ya nane za Ligi Kuu, katika nchi mbalimbali ikiwemo Zambia, Ufaransa pamoja na DR Congo alipo Sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here