Home Burudani IDRIS KUJITANGAZA UK, SA KIKAZI ZAIDI

IDRIS KUJITANGAZA UK, SA KIKAZI ZAIDI

6871
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

MCHEKESHAJI maarufu, Idris Sultan, anatarajia kufanya ziara katika nchi za Afrika Kusini na Uingereza kwa ajili ya kujitangaza kupitia sanaa ya filamu.

Idris amesema mwaka huu mipango yake ni hiyo ya kujitangaza kimataifa, ambapo atakwenda kucheza filamu kwa lugha ya Kiingereza.

“Nina filamu tatu au nne ambazo natakiwa kuzifanya kwa lugha ya Kiingereza, hapa itabidi wabongo wanitenge kidogo, pamoja na lugha ya kigeni naamini kabisa itakuwa sehemu ya kutangaza filamu zetu,” alisema Idris.

Aliongeza kuwa, ni wakati wa wasanii wa Kibongo kuendelea kutumia nafasi zao kuweza kufanya kazi tofauti na kuacha kusubiri kufanyiwa, kwa kuwa ushindani umezidi kuongezeka katika kila idara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here