Home Michezo Kimataifa ISCO, RAMOS WAZUA PRESHA JUVENTUS

ISCO, RAMOS WAZUA PRESHA JUVENTUS

470
0
SHARE

TURIN, Italia

NI siku mbili na saa chache zilizobaki kabla ya Jiji la Cardiff lizizime kwa fainali ya kukata na shoka ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Juventus na Real Madrid, mtanange utakaozikutanisha timu imara zilizopambana vilivyo msimu huu.

Kama ilivyo kawaida, presha ya mchezo inazidi kupanda hadi kwa wachezaji ambapo mastaa wawili wa Juve, Gonzalo Higuain na Giorgio Chiellini wametamka wazi hofu yao juu ya Isco na Sergio Ramos.

Kuna mawili, aidha kocha wa Madrid, Zinedine Zidane amuanzishe Gareth Bale kama atakuwa fiti, lakini pia akamwacha na nafasi yake akacheza Isco. Na kuhusu Ramos, beki huyo anajulikana kwa rekodi yake ya mabao ya dakika za mwisho.

“Bale na Isco ni wachezaji hatari, lakini Madrid ni hatari kwa ujumla. Isco ni zaidi kwa sababu ameongeza vitu vingi ndani ya kikosi chao katika miezi ya hivi karibuni. Kama usipokuwa makini Madrid itakumaliza kama yaliyowatokea Bayern,” alisema Chiellini.

Naye Higuain ambaye anatarajia kukutana na timu yake ya zamani, alisema anamkumbuka na kuutambua uwezo wa hali ya juu alionao Ramos linapokuja suala la kuisaidia timu yake kwa kila hali.

“Soka ndivyo lilivyo, kuna nyakati utajikuta kwenye eneo usilolitarajia; kama kupangwa na Real Madrid halafu wana Ramos. Tunaomba tu asifunge dakika ya 90,” alisema Higuain.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here