SHARE

NA BEATRICE KAIZA,

NYOTA wa filamu anayefanya vema kwenye tasnia ya hiyo, Jackline Wolper, amejipatia umaarufu kupitia kazi zake mbalimbali alizofanya.

Licha ya kuwa mwigizaji mwenye uwezo wa kipekee, pia ni mwongozaji mzuri wa filamu na mwandikaji ‘script’, huku akifanya kazi nyingi na wasanii mbalimbali.

Harmonize ndiye chaguo lake

“Kila binadamu ana haki ya kupenda na kupendwa na pia kila mtu anapenda anapopendwa, mimi na Rajabu ‘Harmonize’ ni wapenzi na ni maamuzi yetu wenyewe kwa maana yeye ndiyo chaguo langu.

Asema waliomtoa

“Kufika kwangu hapa nina watu wa kuwashukuru, kwanza ni Lucy Komba, Ray (Vicent Kigosi), marehemu Steven Kanumba na Mtitu Game, hawa ndio walionitoa kwa maana bila wao nisingejulikana kwenye tasnia ya filamu Afrika Mashariki.

Ndoa na Harmonize

“Kuolewa au kufunga ndoa ni mipango ya Mungu na kila msichana ambaye amefikisha umri wa kuolewa lazima atamani kuwa na ndoa, lakini mimi naamini hilo litafanyika japo kwa sasa nafurahia nafasi niliyopo.

Unywaji pombe na ulevi

“Ni kweli mimi ni mnywaji mzuri wa pombe siwezi kukataa, lakini suala la ulevi si kweli, nakunywa kiasi changu na kuweza kujimudu.

Ushauri kwa wasanii  wachanga

“Kwenye maisha unatakiwa kutokata tamaa, mimi nawashauri wasanii wachanga kwamba wanatakiwa kujituma katika kazi zao pamoja na ubunifu zaidi ili kuwa bora,” anasema Wolper.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here