SHARE

LOS ANGELES, Marekani

HUENDA kuna orodha ndefu ya wasanii wa muziki wa hip hop unaowakubali. Hata hivyo, haijalishi ni wakali kiasi gani, kwa Jay Z watasubiri sana.

Mume huyo wa mrembo Beyonce ndiye kiboko yao si tu kwa kutoa ngoma kali, bali hata kwa hiki alichokifanya hivi karibuni.

Jamaa ametajwa kuwa ndiye rapa wa kwanza kuwa bilionea, kwa mujibu wa ripoti ya Jarida la Forbes lililomtaja kumiliki utajiri wa Dola za Marekani bilioni moja.

Maisha ya kisela utotoni

Unapowazungumzia mastaa waliopitia maisha ya mtaani kabla ya ëkutoboaí, hutaacha kumtaja Jay Z, ikitosha kukwambia aliwahi kusoma shule moja na ëwendawazimuí wengine, Notorious B.I.G na Busta Rhymes.

Kipindi hicho, licha ya kusoma, pia Jay Z alikuwa akiuza dawa za kulevya aina ya cocaine na aliwahi kupigwa risasi mara kadhaa.

Akiwa na umri wa miaka 12 tu, alimpiga risasi kaka yake lakini hakufariki, kisa ni ëbroí kuiba dhahabu zake.

Bifu lake na Nas

Kati ya bifu kali zitakazoendelea kuishi katika kumbukumbu za wapenzi wa muziki wa Hip hop, basi hii nayo imo.

Picha lilianza mwaka 1996, sababu ikiwa ni kitendo cha Nas kutofika studio kuingiza sauti katika wimbo wa Jay-Z, ëBring It Oní.

Hata hivyo, baada ya vita ya maneno kwa muda mrefu, zikiwamo ngoma za kutupiana vijembe, wawili hao walizika tofauti zao mwishoni mwa mwaka 2005.

Atishia kuacha muziki

Mwaka 2003, baada ya Jay Z kuachia albamu yake ëThe Black Albumí, alitangaza kuwa ni mwisho wake wa kufanya muziki.

Alipoulizwa sababu ya kufikia uamuzi wake huo, alisema haoni kama kuna ushindani ulioko miaka mingi iliyopita.

Lakini, baadaye alitengua uamuzi wake huo na hadi leo hii ameendelea kujihusisha na sanaa hiyo licha ya biashara zake nyingi zinazompa mkwanja wa maana.

Ndoa yake yakomesha wadaku

Ilipovuma kuwa Jay Z angeoa, waandishi wa habari za udaku nchini Marekani walitega sikio kila sekunde ya maisha ya msanii huyo.

Wakati huo huo, kumbe mwenzao alishapanga kuwa ingekuwa ndoa ya siri na hakuna hata mwandishi angeweza kuhudhuria.

Sherehe ya ndoa yake na bibiye Beyonce mwaka 2004 ni watu 40 pekee, tena wa karibu, ndiyo waliohudhuria.

Mama yake alivyomliza

Jay-Z amewahi kukiri kulia alipogundua kuwa mama yake mzazi, Gloria Carter, anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Ni ëbi mkubwaí mwenyewe ndiye aliyemwambia mwanawe huyo juu ya suala hilo. Hata hivyo, Jay Z alisema alifurahi kwa kuwa mama yake aliamua kusema ukweli ili kuwa huru.

Baadaye, Jay Z aliliweka wazi hilo katika moja ya ngoma ndani ya albamu yake ya ë4:4:4í.

SHARE
Previous articleJicho la Kagere lipo miguuni!
Next articleUSIKATE TAMAA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here