SHARE

NA MWANDISHI WETU 

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura Mbibo, maarufu kama Lady Jaydee, ameandaa onesho kubwa alilolipa jina la ‘Vocals Night’, ikiwa ni ujio wake mpya wenye lengo la kuwasaidia wanamuziki wanawake.
Onesho hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu, katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Jide alisema tamasha hilo litakuwa la kila mwaka na kwa kuanzia, atashirikiana na wasanii wanne wa kike wa kimataifa ambao ni Juliana Kanyomozi wa Uganda, Zahara Bulelwa Mkutukana wa Afrika Kusini, Damian Soul na Grace Matata wa Tanzania.
“Nina ndoto ya kulifanya onyesho hili kuwa la kila mwaka na lengo lake kubwa ni kutaka kuwakomboa wasanii wanawake ambao wengine wanalazimika kuuza utu wao ili wafanikiwe katika kazi zao, maana kama unavyojua wanaume wameishika hii sanaa karibu kila sehemu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here