SHARE

NA JESSCA NANGAWE
STAA wa Bongomovie Jacob Steven maarufu JB amemkingia kifua Kocha wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Emmanuel Aminike na kutaka asilaumiwe na badala yake timu ijipange upya.


Akizungumza na DIMBA Jumatano, JB alisema, pamoja na kuondolewa katika michuano hiyo mikubwa ya AFCON lakini ni vyema Watanzania wakawa wamoja na kutoa maoni yao ya nini kifanyike na si kutupa lawama kwa kocha.


ìNadhani wengi wamekua wakimtupia lawama kocha, si sawa hata kidogo kwa sisi tunaojua mpira, tunapaswa kujiandaa vyema, Tanzania inahitaji maandalizi kuanzia chini, tumefungwa tukubali matokeo na tujipange upyaîalisema JB.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here