SHARE

NA JESCA NANGAWE

KIKOSI kamili cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Rwanda kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kagame itakayoanza Jumamosi hii nchini humo.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa timu yao itaondoka na wachezaji wote waliosajiliwa lengo kubwa likiwa kutetea ubingwa wao ambao wanaushikilia.

“Tunatarajia kwamba kikosi chetu kitaondoka Alhamis ya wiki hii (kesho), kikiwa na wachezaji wote waliosajiliwa. Sisi ndio mabingwa watetezi hivyo lazima tukapambane kutetea taji letu,” alisema.

Taarifa nyingine kutoka Azam FC zinadai huenda kocha wao mkuu, Etienne Ndayiragije, akatumia michuano hiyo kunasa vifaa vingine vipya kwa ajili ya msimu unaokuja.

Licha ya kwamba wenyewe wanadai wamefunga zoezi la usajili hususan kwa wachezaji wa kigeni huku bado wakibakiwa na nafasi ya mchezaji mmoja tu mzawa, lakini wanaweza wakabadili uamuzi kutokana na namna watakavyopima upepo kwenye michuano hiyo.

“Kwa wachezaji wa kimataifa, tumeshafunga zoezi la usajili na kuhusu hawa wa ndani nafasi ipo ya mchezaji mmoja tu iliyobakia lakini inawezekana maamuzi yakabadilika tutakapofika Rwanda,” alisema kigogo mmoja ndani ya Azam FC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here