SHARE

NA JESSCA NANGAWE

UNAAMBIWA hayo mazoezi wanayofanya Yanga, hao Mwadui FC wanaweza wakajikuta wanapoteana uwanjani kuelekea mchezo wao wa mzunguko wa pili utakaochezwa Jumanne ya wiki ijayo.

Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, watakuwa wenyeji wa Mwadui FC, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumanne usiku wa kuanzia saa 1:00.

Kikosi hicho ambacho kiliondolewa kwenye michuano ya Mapinduzi huko visiwani Zanzibar, kimekuwa kikijifua vikali Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam, kuhakikisha wanaendeleza moto wao wa ushindi.

Akizungumza kuelekea pambano hilo, mratibu wa timu hiyo, Salehe Hafidhi, alisema wanaendelea na mazoezi vyema tayari kwa mchezo huo muhimu kwao huku wakiwa na lengo la kuvuna pointi zote tatu.

“Kikosi kiko vizuri, kinaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Polisi, Kurasini, wachezaji wako katika hali nzuri isipokuwa Raphael Daudi pamoja na Juma Mahadhi ambao wamekua majeruhi lakini wanaendelea vyema.

“Kwa ujumla tunataka tuendeleze rekodi yetu ya kutokufungwa, Jumanne ya wiki ijayo, tutacheza dhidi ya Mwadui Uwanja wa Taifa, utakuwa mchezo mgumu lakini naamini tutavuna pointi tatu,” alisema.

Yanga imeendelea kutawala kwenye msimamo wa ligi ikiwa tayari imejikusanyia pointi 50 huku Azam wakiwa nyuma yao na pointi zao 40, watani zao wa jadi Simba, wakishikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 33.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here