Home Habari JJUUKO AJIFUNGA, MZAMIRU, KICHUYA BADO

JJUUKO AJIFUNGA, MZAMIRU, KICHUYA BADO

2489
0
SHARE

NA SAADA SALIM

SASA mashabiki wa Simba wanaweza kushusha presha zao baada ya beki wao kisiki Mganda Jjuuko Murushid, kusaini mkataba mpya wa miaka miwili huku Mzamiru Yasin na Shiza Kichuya wao wakisubiri.

Mmoja wa marafiki wa karibu na Jjuuko  amelihakikishia DIMBA Jumatano kwamba, beki huyo pamoja na kiungo mshambuliaji Mohammed Ibrahim ‘Mo’ wameongezewa mikataba na sasa ni mali ya Simba.

Alisema suala la wachezaji hao lilifanyika kimya kimya chini ya Bilionea Mohammed Dewji `Mo`,ambapo mkutano mkuu uliofanyika hivi karibuni uliidhinisha kukabidhiwa klabu hiyo kama mwekezaji.

“Si hao tu pia kuna Mzamiru  Yassin na Shiza Kichuya muda wowote kuanzia leo (jana) wataongezewa mikataba mipya kwani hii ya sasa inaelekea ukingoni,” alisema rafiki huyo.

Jjuuko ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakitajwa mara kwa mara kuungana na Yanga, huku ikidaiwa aliwahi kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya mahasimu wao hao, Hussein Nyika nchini Uganda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here