Home Habari JKT RUVU YAWASHA TAA YA KIJANI VPL

JKT RUVU YAWASHA TAA YA KIJANI VPL

710
0
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

TIMU ya JKT Ruvu inayonolewa na kocha Bakari Shime, inaonekana kuwasha taa ya kijani kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kufanikiwa kuvuna pointi 19 katika michezo saba iliyoshuka uwanjani.

Maafande hao juzi Jumatatu walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mshikamano, mchezo uliopigwa Uwanja wa Chamazi Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mtanange huo ulikuwa wa kufunga duru la kwanza kwa ligi hiyo ya daraja la kwanza (FDL) yenye jumla ya makundi matatu, kila kundi likiwa na jumla ya timu nane.

Kwa matokeo hayo yanawafanya JKT Ruvu iliyoko kundi A kuendelea kusalia kileleni na pointi zao hizo 19, wakifuatiwa na African Lyon iliyojikusanyia alama 14, huku Mvuvumwa ikiburuza mkia na pointi zake nne pekee.

Mbali na JKT Ruvu kuwa tishio kwenye kundi lake hilo, lakini katika kundi B, JKT Mlale wapo kileleni wakifungamana na KMC, wote wawili wakivuna pointi 13, huku kinara wa Kundi C akiwa Dodoma FC yenye alama 18.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here