Home Burudani Joh Makini aiweka videoni ‘Perfect Kombo’

Joh Makini aiweka videoni ‘Perfect Kombo’

318
0
SHARE

Joh makiniNA THERESIA GASPER

MSANII kutoka Kampuni ya Weusi, John Simon ‘Joh Makini’, anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Perfect Kombo’ mara baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo ameifanyia nchini Afrika Kusini.

Joh Makini ameliambia DIMBA kuwa yupo katika hatua za mwisho kuikamilisha video hiyo ambayo itakuwa na ubora wa hali ya juu kwa upande wa picha na maeneo aliyotumia kurekodia.

“Nimeona nisubiri Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uishe ndio niachie video hii, hivyo nawaomba mashabiki wangu wawe na subira ya kupata vitu vipya zaidi kupitia wimbo huo,” alisema.

Audio ya wimbo huo ameifanyia nchini Kenya chini ya mtayarishaji R.K Kamani, huku video ikiwa imefanyiwa nchini Afrika Kusini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here