Home Burudani Jokate apambana na ‘panya road’

Jokate apambana na ‘panya road’

802
0
SHARE
Jokate Mwegelo

NA KYALAA SEHEYE,

MWANAMITINDO na ‘Miss Tanzania’ namba mbili (2006), Jokate Mwegelo, amejitosa katika vita ya kupambana na makundi ya kihalifu nchini, ikiwemo ‘panya road’ kwa kuendesha mafunzo yanayoitwa Mother & Child.

Kupitia mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Jokate alisema wazazi wana wajibu wa kuwa karibu na watoto kwa kuwafanya marafiki ili kujua changamoto zinazowakabili, ikiwa ni moja ya njia ya kuwadhibiti wasiangukie kwenye makundi ya kihalifu kama lile la panya road ambalo linatikisa jijini.

“Tunatumia wataalamu mbalimbali wa malezi ya watoto ili wazazi wajue namna ya kuwalea watoto wao, lakini pia kuwafanya marafiki zao kwa ajili ya kuliokoa kundi hilo la vijana kuingia kwenye majaribu ya dunia,” alisema Jokate.

Mafunzo hayo yaliwashirikisha wazazi na watoto kuanzia miaka 8-12 kwa kuwa huo ndio umri mzuri wa mtoto kujifunza kukwepa kuharibika ambapo amepanga kuendesha programu hiyo mara kwa mara, ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kuyaepusha makundi ya vijana kujiingiza kwenye uhalifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here