Home Burudani JOKATE AULA SINEMA ZETU

JOKATE AULA SINEMA ZETU

6422
0
SHARE

Na MWANDISHI WETU


MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, ameteuliwa na uongozi wa Azam Media kuwa mlezi wa tamasha la Sinema Zetu International 2019, linalotarajiwa kuanza Oktoba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Jokate alisema wasanii wanapaswa kuitumia nafasi hiyo kama jukwaa la kutangazia kazi zao pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu sanaa.

ìNiwashukuru Azam Media kwa kunichagua kuwa mlezi wao, niwasihi wasanii kutumia fursa hii ipasavyo, ili kuinua vipaji vyao na kulinda hadhi ya sanaa nchini,î alisema Jokate.

Tamasha hilo limezidi kutanua wigo na kwa msimu huu wa pili litajumuisha nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Mbali ya Jokate, uzinduzi huu ulihudhuriwa pia na wasanii mbalimbali, akiwamo Jacob Steven, maarufu kama JB, Ray, Eshe Buheti, Yusuph Mlela, Natasha na Gabo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here